UCHAWI WA PWANI

 Tuliona katika Afrika uchawi umegawanyika katika sehemu ya bara na pwani, kwa ufupi tulitaja uchawi wa bara tukaonyesha watu wa eneo hilo namna wanavyo tengeneza uchawi wa kifungo na faraka, swali ambalo watu wengi wanauliza, watu wa pwani wanatengenezaje uchawi wa kifungo na faraka?

Kwanza nikiri wazi kuwa pwani kuna uchawi tofauti na bara kwa kuwa katika eneo hilo walipitia wageni kutoka nga'mbo kwa majahazi na meli, baadhi yao waliweka makazi yao katika eneo hilo. Baadhi ya wageni hao ni pamoja na Wareno, Waitali, Waingereza, Wafaransa na Waarabu.

Unakumbuka katika Babeli Iraq ya sasa, alikuwepo mchawi mkubwa aliyeitwa Nimrod aliyezaliwa mwaka 2200- l2154 kabla ya Yesu, bwana huyo alikuwa mfalme aliyeishi wakati wa nabii Ibrahimu, baadaye akajiita Mungu na kuwataka watu wamuabudu.

Aidha unakumbuka katika eneo jirani waliishi Waajemi eneo ambalo kwa sasa inapatikana nchi ya Iran? Watu wa eneo hilo walikuwa wachawi hatari. Katika eneo la Afrika nchini Misri alikuwepo mfalme aliyeitwa Ramses II aliyezaliwa mwaka 1303-1213 kabla ya Yesu, ambaye jina la utawala wao lilifahamika kama Firauni. Firauni tunayemtaja hapa aliishi wakati wa nabii Musa, yeye alikuwa mchawi na aliwaajiri wachawi wa kila aina katika ufalme wake.

Mwandishi Brian Pavlac katika kitabu chake alichokiita Witch Hunts in the Western World: Persecution and Punishment .... anasema: Kuanzia miaka ya 1484 katika nchi za Uholanzi, Ubelgiji, Uswisi, Italia, Ujerumani na Ufaransa nchi hizo zilianzisha kampeni kubwa ya kuwasaka wachawi, wengi waliuawa na wengine walifungwa jela. Hii ni hakikisho kuwa tatizo la uchawi kina muda mrefu na limeathiri Dunia nzima.

Kadhalika Waarabu, Wayahudi na Warumi walibobea katika uchawi, mtu aliheshimika kwa sababu ya uchawi wake. Ni wazi makundi ya watu hawa baadhi yalifika Afrika kwa ajili ya biashara, utafiti na kazi nyingine, na wengine waliweka makazi yao katika maeneo ya pwani.

Pwani upo uchawi wa mizizi ambao ndio wa asili, baadaye walipokea uchawi mpya kutoka kwa wageni, uchawi huo ni pamoja na uchawi wa tarasimu. Tarasimu ni nini? Tarasimu ni maandishi maalumu na michoro iliyoandikwa kwa kufuata hesabu, nyota na kadhalika, hivyo zipo tarasimu za kibabeli, kiajemi, kilatini, kihindi, kiarabu na kichina. Mchawi anapotaka kuloga kwa kutumia tarasimu yenye chapa ya shetani, kwanza huchukua athari za mlengwa kama nyayo, nywele, nyuzi za nguo, kucha au mate. Kadhalika mchawi kwa kutumia shetani anaweza kukipata kimvuki chako wakati wowote na kukifunga katika tarasimu husika.

Tarasimu inapoandikwa huwekwa athali tulizo zitaja kisha husomewa maneno maalumu kwa lugha ya kiajemi, kilatini, kichina, kiingereza cha kale kwa idadi ya jina la mlengwa, na wengine hulisomea kwa lugha ya Kiarabu na hata aya za Quran kwa kuigeuza maana yake, au huanza kusoma kutoka chini kwenda juu. Ili kumfurahisha shetani na majibu yatoke mara mara Moja mchawi bila woga anaweza kuandika aya za Quran kwa kutumia zafarani iliyo changanywa na damu ya hedhi au damu ya paka mweusi au maji ya kuoshea maiti.

Wakati mwingine mchawi huleta sala ya jeuri kwa kusali bila udhu atasali akiwa amesimama mguu moja.  Imeitwa sala ya jeuri kwa sababu yupo tayari Mwenyezi Mungu akamuadhibu siku ya mwisho lakini yeye atimize malengo yake. Wakati mwingine wanaandika tarasimu na baadhi ya maneno ya Quran kwa damu ya mtu, mfano anayetaka afanyiwe uchawi ili amroge jirani yake, rafiki yake, mwanaye, wazazi wake na hata ndugu yake ambaye angeweza kumsaidia, anaambiwa na mchawi atowe damu yake katika kidole ambayo itachanganywa na zafarani kwa ajili ya kuandikia tarasimu.

Tarasimu nyingine huandikwa kwa kuzungushiwa picha ya kiumbe asiyeleweka mwenye kiwiliwili cha kinaadamu chenye sura ya paka au mbwa. Hiyo huitwa tarasimu ya jini.

Tarasimu ya faraka au kifungo cha kichawi, inapoandikwa huletwa kamba iliyookotwa jaani, ambayo hufungwa mafundo 7, 9 au 11 kwa manuizi maalumu na kufungwa katika tarasimu, kisha kuisomea maneno maalumu ili kumwita shetani afike na kukabidhiwa kazi ya kufanya. Kisha tarasimu hiyo hupelekwa katika kaburi la zamani na kufukiwa. Mchawi anapo fika katika kaburi husema "wewe ukiyelala hapa", nimekuletea fulani bini fulani analinga kwa sababu kadhaa wakadha, nataka asifanye chochote juu ya ardhi, kama vile wewe ukivyo kufa na kila kitu chako kimesimama duniani, nataka na Fulani awe mfu kiuchumi, au ndoa yake, au duka lake, kila siku apate mabalaa na mikosi, nimemleta hapa kwako kumfunika na hiki kifuu cha nazi nataka mambo yake yasifanikiwe.

Shetani huituma mionzi ya uchawi huo kwa yule aliye kusudiwa, baada ya siku chache utafukuzwa Kazi, huwezi kupata wateja,  yule jamaa yako wa karibu atakukimbia na hata mkeo au mchumba wako atakuoana wewe ni kituko usiyekuwa na maana yeyote.

0621270517.

Comments

Popular posts from this blog

JINI WA KUTUMWA

Hekima ya Mungu kuumba miti