Hekima ya Mungu kuumba miti
Ili mwanaadamu aweze kuishi salama katika dunia, ili kuwa ni muhimu aendelee kuyatumia madini na bidhaa kadhaa alizoumbiwa, ambazo zinapatikana kwa wingi ardhini. Mwenyezi Mungu kwa hekima kubwa akaotesha miti na majani yanayo fyonza madini na virutubisho kutoka katika udongo.
Mpaka hapo utaona kuna umuhimu kiasi gani kutumia bidhaa za mitishamba katika kuutibu mwili wa mwanaadamu katika kuurudishia mali ghafi za asili alizoumbwa nazo.
Katika makala zetu hizi tutajaribu kutafakari pamoja uzowefu wetu katika siri kubwa aliyoiweka Muumba wetu ndani ya miti pamoja na majani. Kadhalika tutaangalia namna ya kujitibu maradhi yanayotokana na nguvu za giza. Ni ukweli ukiowazi kuwa baada ya Mwenyezi Mungu kumuumba mwanaadamu shetani wa kijini aliumizwa mno kutokana na karama alizotunukiwa mwanaadamu, hivyo aliapa kuhakikisha mpaka mwanaadamu wa mwisho sio atampoteza tu, bali atahakikisha anaishi maishi magumu sana juu ya mgongo wa ardhi.
Shetani ambaye ndiye adui namba moja wa kila mwanaadamu duniani, aliandaa kikosi chake kutoka katika kizazi chake na akafanikiwa kuwapata mawakala wengi kutoka kwa binaadamu mwenyewe, akawafundisha uchawi ambao umekuwa ni sumu kuu katika afya ya mwanaadamu na maisha yake kwa ujumla.
Uchawi umekuwa ni sumu inayo mtenganisha mtu na mwanae, mke na mumewe, bosi na mfanyakazi, mtawala na raia, utashangaa kutokana na uchawi mtoto ambaye amehangaikiwa na wazazi wake kwa muda mrefu sio kumlea kwa shida kubwa tu, amemsomesha na kumtengenezea maisha yake. Lakini shetani kupitia uchawi mtoto husahau mchango wa wazazi wake. Inafikia mtoto anasema bila uoga "Wewe baba au mama kama mngechelewa kunizaa mimi ningekuzaa" Uchawi umeporomisha maadili na kubomoa ndoa nyingi na kutengeneza wimbi kubwa la kijamii.
Dunia inashuhudia ongezeko kubwa la watoto wa mitaani hasa katika nchi za Afrika, ukiangalia namna watoto hao wanavyoishi kama unaimani hata shubiri moja utatokwa na machozi. Kadhalika dunia inashuhudia walemavu wa kila aina, wapo ambao Mungu alikusudia wawe hivyo ili kuonyesha nguvu na mapenzi yake, lakini wengine wameathiriwa na uchawi na kujikuta wakiishi katika ulemavu wa kudumu.
Kadhalika uchawi umeathiri mwili wa mwanaadamu na kusababisha maradhi ya kudumu, hata walipopelekwa Hospitali vipimo vya kisasa vilishindwa kubaini ugonjwa unaowasumbua. Baadhi ya watu hao ni wenye maarifa makubwa waliokuwa wakitegemewa na jamii.
Uchawi umesababisha watu kufirisika, kufungwa jela na wengine kufukiwa katika mashimo ambapo hawatatoka mpaka siku ambayo Mwenyezi Mungu atawaita watu wote, mbele ya mahakama yake kuu ya uadilifu, na Kila kitu katika mahakama hiyo kitabainishwa.
Utaona kuna umuhimu kiasi gani mimi na wewe kujadili swala hili kwa kina. Katika makala hizi tutaangalia namna uchawi unavyotengenezwa na unavyomuathiri mwanaadamu, kadhalika kutaangalia namna ya kujikinga na athari za uchawi na namna ya kujitibu.
Kwa kufunga makala katika sehemu hii ni muhimu kufahamu kuwa uchawi umezienea na kuziathiri jamii zote za mwanaadamu duniani, uchawi unapatikana nchini Marekani, katika nchi za Ulaya, Uarabuni, nchi za Asia kama China, India na nyingine nyingi na hata nchi za Afrika. Ukiangalia janga hili kwa jicho la kitafiti utakubaliana nami kwamba muasisi wa uchawi ambaye ni shetani amejikusanyia wafuasi wengi dunia nzima, na janga hilo sio la Waafrika peke yao.
0621270517
Comments