JINI WA KUTUMWA

 Tulisema upo uchawi wa kila aina, na tulizungunzia uchawi wa kifungo na faraka kutoka bara na pwani.

Sayansi ya kichawi imefanikiwa kutengenezea mapepo na kumtumia mtu, Pepo hilo linaweza kupanda katika kichwa cha aliyelogwa na kuzungumza, na hutumwa kwa nia mbalimbali, mchawi anaweza kutengenezea pepo akaliingiza katika mwili wako ili kufunga kazi zako au kukuletea kila aina ya magonjwa ikiwepo kiharusi.

Pepo ambalo pia huitwa jini wa kutumwa, hutengenezwaje? Kwanza mchawi hutafuta udongo wa kisuguu cheusi, ambacho nchwa wanapandisha udongo mbichi. Udongo huo huchanganywa na mchanga kidogo wa kaburi tatu na mchanga wa njia mbili zinazo pishana (njiapanda) Kisha hutengeneza sanamu linalo lingana na jinsia ya mtu anayetaka kumloga.

Mchawi hutoboa juu ya kichwa cha sanamu Kisha huweka vifaa vya mtu anaye mkusudia, vifaa hivyo ni kati ya nywele, nyuzi za nguo yake, nyayo na kadhalika akikosa hivyo hutumia jina lake tu. 

Kisha hutoboa tumbo na kuweka funza saba wanaotokana na damu ya hedhi iliyooza iliyowekwa kwenye tete, kisha huweka kisiki cha njiani wanachojigonga watu, nzi, kipepeo, mende mweusi, mjusi wa chooni, chura aliyekanyagwa. Baada ya hapo huandika tarasimu na kufunika juu yake.

Baada ya hapo huvalisha sanamu sanda, Kisha hukuchukua sanamu hilo na kulipeleka makaburini usiku wa jumatatu,.......   . ......

Comments

Popular posts from this blog

UCHAWI WA PWANI

Hekima ya Mungu kuumba miti